Child Protection Iringa Tumefanikisha kuunda baraza la watoto Mkoa wa Iringa
- Tumefanikisha kuunda baraza la watoto Mkoa wa Iringa

- Balaza lilizinduliwa kwa sala
- Baraza la Watoto la Halmashauri ya Wilaya limeundwa kwa kuzingatia mwongozo wa mabaraza ya watoto uliuhuishwa juni 2022 na Katiba ya Baraza la Watoto wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
- Wawezeshaji walianza kikao kwa kutoa elimu juu ya haki za mtoto, wajibu wa mtoto, pia watoto waliweza kujadili umuhimu wa baraza la watoto na waliweza kuelewa kuhusu katiba.
- Mada mbali mbali zilitolewa na kiongozi wa baraza la watoto aliomaliza muda wake Scolastika Mwakilisa na father Kindole mzimamizi wa ulinzi na usalama wa mtoto Jimbo la Iringa
- Washiriki wa baraza la watoto wilaya walitoka katika mazingira mbalimbali na wenye historia tofauti ili kuleta uwiano mzuri. Idara na vitengo vinavyo husika walihudhuria na kupata taarifa kamili ya utaratibu wa uchaguzi.
- Jumla ya Tshs 1,470,000/= zilitumika bajeti ya uzinduzi wa baraza.
- Baada ya elimu uchaguzi wa viongozi ulifanyika kwa utaratibu uliozingatia kanuni na sheria zilizomo kwenye katiba. Watoto wote waliridhia utaratibu huo na kufanya uchaguzi kihalali.
- Baada ya uchaguzi, viongozi 6 walipatikana kutoka kata mbalimbali na wataongoza kwa kipindi cha miaka miwili.
Viongozi hao ni;
- Mwenyekiti- ANGELA ROBERT NGANGULI kutoka kata ya ULANDA
- Makamu Mwenyekiti- EMANUELI MWENZI kutoka kata ya MIGOLI
- Katibu – NATHALIA OTUMARY SANGA kata ya KIHOROGOTA
- Mwekahazina- JACKLINE ALEX MTOVE kutoka kata ya IFUNDA
- RESMIDA ZAKARIA- kata ya MAGULILWA
- ELISHA LUKAS MTOVE- kata ya ITUNUNDU
Malengo ya Mafunzo: Malengo mahususi ni:
- Kuwawezesha watoto kuwa na chombo chao cha kutetea haki zao pamoja na kupinga vitendo vyote vya ukatili dhidi yao. Pia kuwasaidia watoto kutambua wajibu wao katika jamii inayowazunguka na hatimae halmashauri ya wilaya ya Iringa kuwa sehemu salama na rafiki kwa watoto kuishi.

