Sera ya Ulinzi wa Mtoto Jimbo la Iringa – Kiswahili

[featured_image]
Download
Download is available until [expire_date]
  • Version 1
  • Download 12
  • File Size 755.53 KB
  • File Count 1
  • Create Date April 10, 2024
  • Last Updated April 10, 2024

Sera ya Ulinzi wa Mtoto Jimbo la Iringa - Kiswahili

Moja ya malengo ya Ndoa ni kupata watoto. Hivyo watoto ni zawadi ya
Mungu kwa familia, ukoo, kabila, taifa na wanadamu wote kwa ujumla.
Ila sasa haitoshi kupata watoto. Jukumu la wote tuliowataja hapo juu ni
kuwalea na kuwatunza na kuwalinda watoto. Hizi ni haki zao za msingi.
Upendo kwa watoto ni dalili ya ukomavu wa walezi wote.
Kristo Yesu alikuwa mtoto ndani ya familia ya Maria na Yosefu. Kwao hao
wawili alijifunza maana ya upendo, yaani kujali nafsi za wenzetu kwa pendo
la dhati.
Kwa vile dunia ya leo ina ukengeufu uliozagaa wa haki za mtoto imelazimu
kujiwekea sera na miongozo itakayosaidia ulinzi wa mtoto na utetezi wa haki
zake. Hivyo mtoto atakua akiwa na furaha na ubinadamu wenye baraka na
amani na akili komavu.
Mungu atulindie watoto wetu walio Taifa na Kanisa la kesho. Tukiwatendea
mema watatukumbuka na kutuombea mbele za Mungu.