Kikao na Kamati ya Ulinzi wa Mtoto pamoja na Askofu wa Jimbo




Katika mwaka huu, Idara ya Ulinzi wa Mtoto ilifanikiwa kufanya kikao maalum na Kamati ya Ulinzi wa Mtoto pamoja na Mhashamu Askofu wa Jimbo la Iringa.
Kikao hiki kilikuwa na lengo la:
- Kuitambulisha Kamati na kuiidhinisha. Katika kikao hicho aliwashukuru wajumbe kwa kufika na alisisitiza umuhimu wa ulinzi wa mtoto na kwamba kamati hii ifanye majukumu yake kadiri inavyotakiwa.
- Kutathmini hali ya ulinzi na malezi ya watoto ndani ya Jimbo
- Kujadili changamoto zinazowakabili watoto katika jamii
- Kuweka mikakati mipya ya kuimarisha ulinzi wa mtoto kwa mwaka unaofuata
- Kuongeza ushirikiano kati ya Kanisa, familia, shule, na serikali
Kikao hicho kilisisitiza umuhimu wa kila mzazi, mlezi, na kiongozi wa Kanisa kuwa mstari wa mbele katika kulinda watoto dhidi ya ukatili, unyanyasaji, na mazingira hatarishi.